
Anaitwa
Casto kijana kutoka
Clouds TV na hapa tulikuwa tukifanyiwa Interview ya kipindi chake kipya ambacho kitazinduliwa soon na kitatambulika kwa jina la
20 za Town ambacho kitakuwa kikirushwa kila Jumamosi usiku Clouds TV. Kipindi hiki kitakuwa kinazungumzia Bongo Fleva pamoja na videos za bongo na bila kusahau Interview kwa wadau wote wa mziki huu wa bongo fleva

Alianza na mimi kwa kuniuliza maswali tofauti tofauti juu ya blog yangu na mambo mengine mengine ambayo majibu yake yalikuwa mepesi kuyajibu. Location hii ilikuwa pale
Mlimani City.


Baada ya hapo tukaelekea kwa msanii
Young D kutoka
Fish Crab naye alikuwa akiulizwa maswali ya kimziki zaidi pamoja na mziki anaoufanya kama yeye anauchukuliaje kwa miaka ya baadae. Location hii ilikuwa pale
Ubungo Plaza

Show ya Casto ikaishika kwa msanii mwingine anayejulikana kwa jina la
CPWAA, huyu yeye alikuwa akiulizwa juu ya video mpya aliyoitoa ambayo inaitwa
So Pwaa. Hapa maswali yalikuwa ya kawaida na mtu mzima Cpwaa aliyamudu kuyajibu. Location ilikuwa pale
Mbalamwezi Beach

Vijana kutoka mjengo Clouds TV hawa hapa,
Casto, Raymond &
Joram
No comments:
Post a Comment