Jamaa anaitwa Phaustine Leonce Village aka Phaleville kutoka Ikungi Singida Vijijini .Lakini yupo hapa jijini Darisalaam maeneo ya Standi ya Mwenge karibu kabisa na Baa ya Kilimanjaro.Ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya na amewahi kurekodi traki kibao zikiwemo Chap Chap ikiwa kashirikishwa Nick Maujanja , Macho Kwenye aambayo kashirikishwa Chingchilla na Ni Money Tu aliyomshirikisha King K.
Traki nyingine ni Huwezi kashirikishwa jamaa kutoka Kenye anayeitwa Slim G na Njoo Home wamechana Jux Vuitton na Mwala B .Traki tatu za mwanzo zimetayarishwa na Profesa Ludigo na ya mwisho kafanya Maneke.
"Licha ya kudili na ya muziki , lakini pia mimi ni mfanya biashara na hapa ndio ofisini kwangu , siunacheki pamba za kila aina zipo ?
Miezi michache ijayo natarajia kuikuza Crunk kwa kufungua matawi hadi huko mikoani kwani niwateja wengi hivyo nimepanga kuwarahisishia huduma ."Alisema msanii huyu ambaye ni mjasilia mali kweli kweli .
Kwa watu ambao wanataka kuwasiliana naye ni kwamba namba hii:
0717-077089
No comments:
Post a Comment